Pages

Saturday, March 22, 2014

A TRUE SCHOOL HIP-HOP MUSIC VIDEO LAUNCH @GREEN LOUNGE THIS SUNDAY 23.03.2014



Monday, March 10, 2014

CHEGE,MADEE NA B 12 WAFUNIKA MBEYA TAMASHA LA COCA COLA






Meneja masoko wa Cocacola Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Rashid Mgonja alisema  kampuni hiyo pamoja na kuungana na Watanzania katika kuadhimisha siku ya Wanawake duniani pia wamezindua kampeni inayojulikana kwa jina la Good time na Cocacola





Mwanamke Hadhara Njelya mwenye uwezo wa kuchezea mpira jinsi atakavyo kutoka Jijini Mbeya.

Add caption


KAMPUNI ya vinywaji baridi ya Cocacola Kanda ya Nyanda za juu kusini imeungana na Dunia nzima kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani kwa kuandaa burudani kubwa iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe Jijini Mbeya.
Burudani hizo zilipambwa na Wasanii kutoka ndani ya Mkoa wa Mbeya walioonesha vipaji vyao akiwemo Mwanamke Hadhara Njelya mwenye uwezo wa kuchezea mpira jinsi atakavyo kutoka Jijini Mbeya.
Mbali na vipaji hivyo vya Mkoa wa Mbeya pia burudani kabambe zilitolewa kutoka kwa wasanii wakubwa wa Jijini Dar Es Salaam ambao ni pamoja na Wasanii kutoka kundi la Wanaume Chege na Temba pamoja na Madee  huku mwendesha sherehe (MC)akiwa ni mtangazaji wa kituo cha Redio cha Clouds fm kipindi cha XXL, B12.
Akizungumzia tukio hilo, Meneja masoko wa Cocacola Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Rashid Mgonja alisema  kampuni hiyo pamoja na kuungana na Watanzania katika kuadhimisha siku ya Wanawake duniani pia wamezindua kampeni inayojulikana kwa jina la Good time na Cocacola.
Alisema lengo la kampeni hiyo ni kujenga mahusiano, kuwaunganisha Watanzania na kuwajengea uwezo wajasiliamali wadogo kupitia vinywaji vya Cocacola kutokana na kuuza bidhaa hizo kwenye maduka yao ambapo kampuni hiyo itaweza kuwapa Majokofu na vifaa vingine vya kufanyia biashara.
Mgonja alisema Kampeni hiyo ni ya Kitaifa ambayo ilianza rasmi Februari 16, Mwaka huu ambapo Kampuni hiyo imejiwekea mikakati kuhakikisha hadi Mwaka 2015 inawanufaisha wajasiliamali wapatao 30,000 kwa Kanda ya Nyanda za Juu pekee ambapo hadi sasa imewanufaisha wajasiliamali 15,000

Monday, March 3, 2014

MWANZA NA MBEYA WAULA NA PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI


 Mshindi wa Samsung Galaxy tab3 kutoka Tunduma Mbeya Vedastus Kalinga akionesha zawadi yake mara baada ya kukabidhiwa mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti kanda ya kusini Lumuli Msika(kushoto)akimpongeza mmoja wa washindi wa promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti Julius Chao kutoka Mbeya mara baada ya kumkabidhi king'amuzi katika hafla fupi iliyofanyika jijini Mbeya.
 Meneje Masoko wa eneo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Charles Masonga(kushoto) akimkabidhi zawadi ya king'amuzi mmoja wa washindi wa promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti  Deus P. Mwikitalu kutoka Buhongwa jijini Mwanza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki,anayeshuhudia ni Meneja Mauzo wa eneo hilo. 
Meneje Masoko wa eneo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Charles Masonga (kushoto) akimkabidhi zawadi ya simu aina ya samsung Galaxy tab3 mmoja wa washindi wa promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti Mwl. Jacob Nnko, 36,kutoka Nansio Ukerewe katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa wiki

FAINALI ZA NYAMA CHOMA JIJINI MBEYA, NEW CITY PUB WAIBUKA MABINGWA



Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Dk.Samweli Lazaro (katikati) na jaji Mkuu wa mashindano ya Safari Nyama Choma, Lawrence Salvi (kulia) wakimkabidhi zawadi ya Kombe na fedha taslimu Shilingi milioni moja(1,000 000) mpishi Mkuu wa New City Pub, Geofrey Mwashilindi mara bada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma 2014 yaliyojanyika katika Viwanja vya CCM Ilomba Mkoani Mbeya mwishoni mwa wiki .Wapili kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo na Meneja wa Tawi la TBL Kanda ya Kusini, Vivianus Rwezahula.
Mpishi Mkuu wa New City Pub, Geofrey Mwashilindi akishangilia na kitita cha Shilingi milioni moja(1,000 000) mara baada kibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Nyama Choma 2014 kwa Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika CCM Ilomba mwishoni mwa wiki .Kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa mashndano hayo, Lawrence Salvi,Meneja wa bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mbeya, Sameli Lazaro, Meneja wa Tawi la Tbl Kanda ya Kusini, Vivianus Rwezahula na Meneja mauzo na matukio Tbl Mbeya, Clauds Chawene.
Mashabiki wa New City Pub wakiwa wamembeba juu mpishi mkuu wa pub hiyo, Geofrey Mwashilindi mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya Safari Nyama Choma 2014 kwa Mkoa wa Mbeya yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Ilomba mwishoni mwa wiki.
Mashabiki na wapishi wa New City Pub wakishangila ndano ya gali lao aina ya Pic up yenye namba za usajili T952 BFB wakielekea kwenye Pub yao mara baada ya kuibuka mabingwa wa Safari Nyama Choma 2014 yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Ilomba mwishoni mwa wiki