Add caption
KAMPUNI ya vinywaji baridi ya Cocacola
Kanda ya Nyanda za juu kusini imeungana na Dunia nzima kuadhimisha Siku ya
Wanawake duniani kwa kuandaa burudani kubwa iliyofanyika katika viwanja vya
Shule ya Msingi RuandaNzovwe Jijini Mbeya.
Burudani hizo zilipambwa na Wasanii
kutoka ndani ya Mkoa wa Mbeya walioonesha vipaji vyao akiwemo Mwanamke Hadhara
Njelya mwenye uwezo wa kuchezea mpira jinsi atakavyo kutoka Jijini Mbeya.
Mbali na vipaji hivyo vya Mkoa wa Mbeya
pia burudani kabambe zilitolewa kutoka kwa wasanii wakubwa wa Jijini Dar Es
Salaam ambao ni pamoja na Wasanii kutoka kundi la Wanaume Chege na Temba pamoja
na Madee huku mwendesha sherehe (MC)akiwa ni mtangazaji wa kituo cha
Redio cha Clouds fm kipindi cha XXL, B12.
Akizungumzia tukio hilo, Meneja masoko
wa Cocacola Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Rashid Mgonja alisema kampuni
hiyo pamoja na kuungana na Watanzania katika kuadhimisha siku ya Wanawake
duniani pia wamezindua kampeni inayojulikana kwa jina la Good time na Cocacola.
Alisema lengo la kampeni hiyo ni kujenga
mahusiano, kuwaunganisha Watanzania na kuwajengea uwezo wajasiliamali wadogo
kupitia vinywaji vya Cocacola kutokana na kuuza bidhaa hizo kwenye maduka yao
ambapo kampuni hiyo itaweza kuwapa Majokofu na vifaa vingine vya kufanyia biashara.
Mgonja alisema Kampeni hiyo ni ya
Kitaifa ambayo ilianza rasmi Februari 16, Mwaka huu ambapo Kampuni hiyo
imejiwekea mikakati kuhakikisha hadi Mwaka 2015 inawanufaisha wajasiliamali
wapatao 30,000 kwa Kanda ya Nyanda za Juu pekee ambapo hadi sasa imewanufaisha
wajasiliamali 15,000
|
No comments:
Post a Comment