Kundi
la Kwanza la Washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya pili ya Mchujo
katika Mashindano ya Tanzania Movie Talents Mkoani Mbeya Wakipewa
maelekezo kwaajili ya kuanza hatua ya mchujo leo.
Washiriki
wa Shindano la Tanzania Movie Talents Mkoani Mbeya kanda ya Nyanda za
Juu Kusini wakiwa katika mazoezi mara baada ya kukabidhiwa Muswada
(script) ikiwa ni hatua ya pili sasa ya shindano hili
Ngoja tuangalie wenzetu wanafanyaje.....
Wakitafakari muswada (script)..
Washiriki
wakiendelea kuusoma Muswada (Script) kwa makini mara baada ya
kukabidhiwa kwaajili ya hatua ya pili ya Shindano la Tanzania Movie
Talents Mkoani Mbeya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.Picha zote na
Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mbeya
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mbeya
Leo
Shindano la Tanzania Movie Talents limeingia ya hatua ya pili ya mchujo
ambapo washiriki 30 wanatakiwa kupatikana kwaajili ya hatua ya tatu,
washindi 30 watakaopatikana leo katika hatua hii ya pili wataendelea na
hatua ya tatu ambapo washiriki
15 ndio watachukuliwa kwaajili ya kuendelea na mashindano hayo na
hatimaye kupatikana washindi watatu bora ambao watawakilisha kanda ya
nyanda za Juu Kusini na kwa kila mshindi mmoja kuibuka na kitita cha
shilingi laki tano (500,000/=).
Mpaka sasa majaji wanaendelea kutafuta washiriki 30 watakaoendelea na shindano hilo kwa kanda ya nyanda za Juu Kusini na hatimaye kesho washindi watatu watapatikana na kuiwakilisha kanda ya kanda ya nyanda za Juu Kusini katika
fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na hatimaye mshindi
katika fainali hiyo kujinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 za
kitanzania (50,000,000/=)
Shindano la Tanzania Movie Talents linatarajiwa kumalizika kesho katika kanda ya nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya
na hatimaye kuhamia Kanda ya Kusini ambapo usaili utafanyika Mkoani
Mtwara na wakazi wa Kanda ya Kusini wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili
kuweza kuonyesha vipaji vyao na kuweza kuitumia fursa hii, Vilevile fomu
za usaili zitapatikana Siku hiyohiyo ya usaili na fomu hizo hazina
gharama yoyote ile.